
Mahakama ya Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera imemuhukumu kifungo cha miaka 20 jera Eziboni Mujuni Albogast (29) mkazi wa Kijiji cha Bunazi Wilaya ya Misenyi kwa kosa la kuharibu miundombinu ya umeme yenye thamani ya shilingi milioni 11,536357.35.
Akisoma hukumu hiyo hakimu Mkazi Mkuu na Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Muleba Bw. Daniel Nyamkerya amesema kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo julai 21 mwaka 2024 katika Kijiji cha Nyakamahama Wilayani Muleba ambapo aliharibu nguzo za umeme tatu, nyaya, kifaa cha kuchimba shimo la nguzo na vifaa vingine vya umeme.
Bw. Nyamkerya amesema kuwa mtuhumiwa alikutwa eneo la tukio akiwa na wenzake wawili ambao walitoroka ndipo yeye alipelekwa kituo cha polisi Kamachumu ambapo upande wa mashitaka umethibitisha pasipo kuacha shaka hivyo amehukumiwa kifugo cha miaka 20 kutumikia jera.
Awali mwendesha mashitaka Bw. Cyrillo Baltazar ameiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshitakiwa ili kukomesha vitendo vya uharibifu miundombinu ya Serikali.