Al Hilal ya Sudan imewasilisha malalamiko rasmi CAF dhidi ya RS Berkane kuhusu ushiriki wa beki Hamza El Moussaoui kwenye mchezo wao wa hivi karibuni.
Malalamiko ya Al Hilal dhidi ya RS Berkane
• Kashfa ya Matumizi ya Dawa za Kusisimua Misuli: El Moussaoui alikuwa amefungiwa siku 30 baada ya kufeli vipimo.
• Utata wa Muda: CAF ilithibitisha adhabu hiyo siku mbili kabla ya mechi, lakini ghafla kifungo kiliondolewa siku ya mchezo!
• Mchezaji huyo ndiye aliyesababisha penalti iliyoipa Berkane bao la kusawazisha.
Al Hilal inashikilia kuwa mchezaji huyo hakuwa na sifa za kuingia uwanjani na tayari wamewasilisha ushahidi mzito.

Endapo CAF itajiridhisha kuwa kulikuwa na udanganyifu huo, RS Berkane inaweza kupoteza mchezo huo.
Haya ni matokeo ya mechi ya Al Hilal Vs RS Berkane
Mkondo wa Kwanza (Machi 14, 2026):
RS Berkane 1 – 1 Al Hilal
Mchezo ulipigwa Morocco.
Al Hilal walitangulia kufunga, lakini Berkane ilisawazisha kwa penalti dakika za majeruhi (90+9′).
Mkondo wa Pili (Machi 22, 2026):
Al Hilal 0 – 1 RS Berkane
Mechi ilipigwa Kigali, Rwanda (Uwanja wa nyumbani wa Al Hilal).
RS Berkane ilishinda kwa bao la dakika ya 93.
Matokeo ya jumla (Aggregate): RS Berkane 2 – 1 Al Hilal
RS Berkane ikafuzu kwenda hatua ya nusu fainali.
