
Na, Zawadi Bashemela
DODOMA
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Jumanne Abdallah Sagini amesema sheria ya kudhibiti pombe za asili ya mwaka 1968 haitambui pombe aina ya Gongo kama pombe ya asili.
Amesema kwa mujibu wa sheria hiyo, mtu anayekusudia kutengeneza ama kuuza pombe ya asili anapaswa kuomba leseni katika mamlaka ya serikali za mitaa.
Sagini amesisitiza kuwa pombe aina ya Gongo, Machozi ya Simba, Moshi ama Umeme inawezwa kutengenezwa kwa kuzingatia sheria.