
Askofu wa kanisa la kiinjili la kirutheri Tanzania dayosisi ya kaskazini magharibi dkt. Abedinego Keshomshahara amewataka wahitimu wa tasisi ya sayansi ya afya Ndolage kuwa mabalozi wazuri kwa kutoa huduma bora kwenye jamii kwa kuzingatia miongozo iliyowekwa na wizara ya afya.
Askofu Keshomshahara amesema hayo katika mahafari ya 68 ya chuo cha Tasisi sayansi ya afya Ndolage kilichopo Kata ya Kamachumu Wilayani wilayani humo wakiwa jumla ya Wanafunzi 85 ambao wamehitimu kozi mbalimbali za uuguzi na ukunga, utabibu, ustawi wa jamii na famasia.
Naye Katibu tawala Wilaya ya Muleba Bw. Benjamin Mwikasyege ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafari hayo amesema Serikali ya itaendelea kushirikiana na wawekezaji wa tasisi za afya kutatua changamoto za uhaba wa watumishi na vifaa tiba katika hospital za binafsi na dini ili kuendelea kutoa huduma Bora za afya kwa kuzingatia miongozo inayotolewa na Wizara ya afya.