MUKULU SJ

John Francis Mukulu SJ ni Mmjezuiti na mhandisi mzoefu wa mifumo ya TEHAMA. Ana BSc ya Sayansi ya Kompyuta, PGD na MA ya Falsafa kutoka Arrupe Jesuit University, MSc ya Sayansi na Uhandisi wa Kijani kutoka Chuo Kikuu cha Sophia, Japan, na anasoma PhD akijikita katika maadili ya Akili Mnemba (AI Ethics). Amewahi kuwa mhandisi mkuu UDSM, mtaalamu wa DHIS2 na mifumo ya Linux.