
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa ameliagiza Jeshi la Polisi kumtafuta na kumhoji aliyeandika kwenye mitandao ya kijamii kuwa “siku za Kitima zinahesabika’ pamoja na watu wote waliohusika na uhalifu huo, kisha kuchukua hatua kali za kisheria.
Bashungwa pia ameagiza kusakwa na kukamatwa kwa alitetengeneza na kusambaza Waraka Feki wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), kwa kuwa ulilenga kuzua taharuki kwa umma.
Bofya hapo kusoma Tamko la TEC pamoja na Walaka Feki ⬇️
“Naliagiza Jeshi la Polisi kumtafuta kwa haraka, yule mtu aliye-tweet kwenye mitandao ya kijamii kwamba,” siku za Kitima zinahesabika, na hatua kali za kisheria zichukuliwe haraka iwezekanavyo, kwa watu wote watakaobainika kuhusika katika tukio hilo,”amesema Bashungwa.
Aidha, amelaani tukio la kushambuliwa kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Padri Dk. Charles Kitima, lililotokea majira ya saa nne usiku Aprili 30, 2025 katika makao makuu ya TEC, Kurasini jijini Dar es Salaam.