
Halmashauri ya wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera kupitia idara ya maendeleo ya jamii imewataka wanawake, vijana na makundi maalumu kujitokeza kuomba mikopo ya asilimia 10 inayotolewa halmashauri.
Afisa mikopo idara ya maendeleo jamii wilaya ya Biharamulo Bw. Dirra Sila amesema hayo wakati akitoa elimu juu ya umhimu wa vijana, wanawake na wenye ulemavu kujikwamua na umasikini.
Amesema kabla vijana, wanawake na wenye ulemavu kuchukua mikopo kwa ajili kuendeleza maisha yao ni muhimu kufanya kazi kwa kujituma ili kutimiza malengo yao.
Afisa Mikopo Biharamulo- Dirra Sila
Baadhi ya wanawake waliohudhuria mafunzo hayo Bi. Happines Emanuel na Jasmini Yona wamesema maafisa maendeleo ya jamii wanatakiwa kuendelea kutoa elimu kwa wanawake na vijana hasa wa vijiji ili waweze kunufaika na fursa zinazotolewa na serikali.