
Serikali imetenga shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa maji taka katika wilaya ya Chato mkoani Geita ili kuimarisha afya za wananchi.
Mkurugenzi wa mamlaka ya maji mjini humo mhandisi Izack Mgeni amesema kwa sasa wilaya ya Chato haina huduma ya maji taka na badala yake wakazi wa wilaya hiyo huipata katika wilaya jirani za Geita na Muleba mkoani Kagera.
Amesema kwa kutambua changamoto hiyo tayari utekelezaji wa kusanifu mradi wa maji taka umeanza kutekelezwa katika kata ya Katende na mpaka sasa wamefikia asilimia 40 na baada ya kukamilika utawahudumia wakazi wa wilaya ya Chato na maeneo jirani.
Baadhi ya wakazi wa Chato akiwemo Kamese Malima, Samson Tito na Yudes Petro, wamepongeza hatua ya utekelezaji wa mradi huo na kusema kuwa baada ya kukamilika wataondokana na gharama wanazotumia kukodi magari kwa ajili ya huduma ya maji taka.