Rapa lord eyes mweusi ameibua mjadala mtandaoni baada ya kumjibu kwa ukali chidbenz, kufuatia kauli ya Chid Benz aliyodai kuwa Lord Eyes hana ngoma yake mwenyewe inayojulikana zaidi ya zile alizofanya na Weusi na Nako2Nako.
Lord Eyes alijibu kwa kusema kuwa hata Chid Benz, tangu atoke kwenye matatizo yake ya zamani, hana wimbo wowote mkubwa uliotikisa.
Pia alitaja baadhi ya ngoma zake zinazotambulika, akisisitiza kuwa hata zile za Weusi na Nako2Nako ni sehemu ya kazi zake, kwa sababu alihusika kikamilifu katika kuzifanya ziwe kubwa.