Mwigizaji na msanii wa mapigano ya kijeshi na judo, Chuck Norris alifariki dunia jana asubuhi akiwa na umri wa miaka 86, familia yake imetangaza kupitia mtandao wa Instagram.
Taarifa zinaeleza kuwa Norris alilazwa hospitalini huko Hawaii kwa dharura ya kimatibabu kabla ya kifo chake.
Katika taarifa yao, familia yake imesema “Tunajua wengi wenu mmesikia kuhusu kulazwa kwake hospitalini hivi karibuni, na tunashukuru sana kwa maombi na usaidizi mliompa, hamkuwa mashabiki tu, mlikuwa marafiki zake”
Tunasikitika kama familia kutangaza kifo cha ghafla cha mpendwa wetu Chuck Norris kilichotokea jana asubuhi. Ingawa tungependa kuweka hali hiyo kuwa ya faragha, tafadhali jua kwamba alikuwa amezungukwa na familia yake na alituacha akiwa na amani.
“Kwa ulimwengu, alikuwa msanii wa mapigano ya kijeshi na judo, mwigizaji, na nembo ya nguvu. Kwetu, alikuwa mume aliyejitolea, baba na babu mwenye upendo, ndugu wa kipekee, na kitovu cha familia”
