Maelezo ya Kipindi
Connector ni kipindi cha burudani maalumu kinacholenga vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 35. Lengo kuu la kipindi hiki siyo tu kuburudisha bali pia kuwawezesha vijana kutimiza ndoto zao katika tasnia ya muziki na kukuza vipaji vingine walivyonavyo. Kipindi hiki huwashirikisha wasanii maarufu, hivyo kupanua upeo wa vijana katika masuala ya muziki kupitia mahojiano maalumu pamoja na vipindi mubashara studio.


Muda wa Kipindi
Kipindi hiki hurushwa hewani Jumatatu hadi Ijumaa, kuanzia saa 8:00 mchana hadi saa 10:00 jioni.
Mfumo wa Kipindi
Kipindi cha Connector kina sehemu kuu zifuatazo:
- Kufungua na Kujitambulisha (14:00 – 14:15 Mchana)
- Utambulisho rasmi wa kipindi huku ukianza na wimbo moja maarufu uliyochaguliwa kwa umakini ili kuwavutia wasikilizaji.
- Chapa za DJ (14:15 – 14:45 Mchana)
- Burudani maalumu kutoka kwa DJ wa studio, ikiwa ni mchanganyiko wa muziki wa aina mbalimbali unaopendwa na vijana.

- Scanner (15:00 – 15:30 Mchana)
- Kuscan taarifa za kiburudani zinazotrend mtandaoni
- Interview na wasanii wakubwa na wachanga
- Mada zinazomuelimisha na kumjenga kijana
- Chapa za Wana (15:00 – 15:45 Mchana)
- Wasikilizaji wanachagua nyimbo muda wa kipindi kupitia sms na dj anazicheza.
- Nipe Tano (15:45 – 15:55 Mchana)
- Ujumbe mzuri kutoka mtandaoni, au kutoka kwa mtu mwenye ushawishi unaoelimisha, unaochekesha lakini ndani yake Kuna kitu mtu anajifunza.
Upekee na Umuhimu wa Kipindi
Kipindi cha Connector ni cha kipekee kutokana na muundo wake wa kuburudisha na kuelimisha kwa wakati mmoja. Ni jukwaa muhimu kwa vijana kujifunza kutoka kwa wenzao na wasanii wakubwa waliofanikiwa. Mahojiano ya wasanii maarufu pamoja na burudani za moja kwa moja huongeza hamasa na mvuto wa kipindi. Kipindi hiki pia kinafanyika mara kwa mara katika mfumo wa matangazo ya nje (Outside Broadcast – OB), hivyo kutoa fursa zaidi za matangazo na udhamini.
Walengwa wa Kipindi
Kipindi cha Connector kinalenga vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 35, lakini kutokana na umaarufu wake, kipindi hiki pia hupendwa na kusikilizwa na watu wazima. Kipindi hiki ni maarufu kwa vijana wanaotaka kujua zaidi kuhusu tasnia ya burudani, michezo, na maisha ya mastaa.

Nafasi ya Wadhamini (Matangazo na Ushirikiano)
Kutokana na umaarufu wake mkubwa kwa vijana na watu wazima, Connector ni kipindi chenye nafasi kubwa kwa matangazo mbalimbali, hasa kwa bidhaa na huduma zinazowalenga vijana. Wadhamini wanaweza kuweka matangazo ya kipekee au kushirikiana na wadhamini wengine kupitia sehemu mbalimbali za kipindi. Pia, kipindi hutoa fursa ya matangazo ya nje ambayo yanaongeza wigo wa matangazo na ushawishi.

