Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Asha-Rose Migiro amesema vijana nchini wana paswa kuilinda Tanzania kwa kuwa ni Taifa lao.
Dkt. Migiro ametoa kauli hiyo leo mkoani Dodoma, wakati wa Jukwaa la Wanawake 2025 linalolenga kujadili mchango wa amani kwa Taifa.
Amewataka vijana nchini kufanya kila linalowezekana kuhakikisha Taifa haliingii katika changamoto kama zilizojitokeza siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025.
Jukwaa la Amani la wanawake limefanyika likiwa na kaulimbui ya Mama ni mama ikiwa ni mwendelezo wa kuhakikisha amani ya nchi ina kuwa kipaombele kwa taifa kudbiti yaliyotokea Oktoba 29 2025.