Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika CAF, Dkt. Patrice Motsepe, amesema msimamo wa CAF ni kwamba michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) itafanyika katika mataifa ya Tanzania, Kenya na Uganda mwaka 2027
Dkt. Motsepe ameyasema hayo leo Februari 13, 2026, jijini Dar es Salaam na kwamba uvumi unaosambazwa mitandaoni kuwa mataifa hayo hayako tayari kuandaa mashindano hayo hauna ukweli.
Amesisitiza kuwa AFCON 2027 itakuwa na mafanikio makubwa zaidi katika historia akiongeza kuwa Tanzania, Kenya na Uganda zilijipambanua vizuri kwenye michuano ya CHAN, hivyo hakuna sababu ya kupokonywa nafasi ya kuwa wenyeji wa AFCON 2027.
Aidha, amewataka viongozi wa mataifa hayo kuendelea kushughulikia changamoto za miundombinu ili kuhakikisha mashindano yanafanyika bila kasoro.
