Soko la Hisa la Dar es Salaam ni Mwanachama wa Masoko ya Hisa ya Dunia, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi amekutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Peter Nalitolela.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo Ijumaa Februari 13, 2026, jijini Dodoma.
Katika Mazungumzo hayo, Dkt. Nchimbi amewahimiza watendaji wa DSE kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuwa wabunifu katika masuala ya masoko na kuendelea kuvutia uwekezaji.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa DSE, Peter Nalitolela ameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutafuta mitaji ili kuweza kusaidia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ya kufikia uchumi wa Dola 1 trilioni za Marekani ifikapo mwaka 2050.
Thamani ya jumla ya Soko la Hisa la Dar es Salaam ni Sh31.9 trilioni, ikiwa na jumla ya wawekezaji waliosajiliwa 779,000
