
Na, Jerome Robert
BUKOBA
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro amewataka Watanzania kupuuza maneno ya wa wanasiasa wanaopita maeneo mbalimbali nchini na kueneza habari za uchochezi kuhusu Uchaguzi Mkuu.
Ndumbaro amesema hayo leo wakati wa ufunguzi wa kampeini ya kisheria katika Mkoa wa Kagera iliyofanyika katika viwanja ya Mayunga vilivyopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
Ndumbaro amesema kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeeleza sababu zinazoweza kusababisha Mtanzania kutoshiriki uchaguzi na imebainisha uchaguzi kama haki ya msingi ya kila mwananchi mwenye umri wa kuanzia miaka 18.
Aidha, mamia ya wananchi wamejitokeza kupeleka changamotoo zao za kisheria na kuziwasilisha kwa wanasheria na wengine kupata fursa ya kukabidhiwa mawakili mbele ya waziri huyo.