Rapa Tanzania fidq amehamia kwenye tasnia ya utayarishaji wa muziki baada ya kupata ajali mwaka huu wa 2025.
Fidq amesema kupata ajali haikuwa sababu ya kumfanya yeye akate tama hivyo aliamua kuendelea kupambana Zaidi. Kupitia ukurasa wake wa Instagramu Ngosha amesema mwaka 2025 ulimjaribu, alipata ajali, lakini badala ya kunyong’onyea, aligeuza utayarishaji wa muziki kuwa liwazo lake.
Fid ameeleza kuwa ajali hiyo ilimlazimu kuingia katika kipindi cha kujitenga kwa miezi mitatu, muda alioutumia kupona, kutafakari na kujijenga upya.
Katika kipindi hicho kigumu, Fid Q amesema hakukata tamaa, bali aligeukia muziki kama njia ya kujitibu kisaikolojia.
Akiwa peke yake, alianza kujifunza na kujihusisha zaidi na utengenezaji wa midundo (beat making), jambo lililoanza kama tiba lakini baadaye likageuka kuwa dhamira mpya ya maisha.
Fid Q amezindua rasmi kazi yake ya kwanza aliyoiandaa kama mtayarishaji, wimbo huu amemshirikisha mmoja wa wasanii anaowapenda na kuwaheshimu zaidi, @damiansoulmusic.
Kwenye Hiphop amefanya karibu yote na kupewa heshima kama mmoja ya rappers bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania, lakini sasa anakwenda kuitafuta legacy nyingine kama mtayarishaji wa muziki.