
Wananchi wa jiji la Mwanza wamesema wataiunga mkono serikali ambayo itajali haki, sheria pamoja na uwajibikaji wao kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi oktoba mwaka huu
Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Radio Kwizera baada ya mkutano wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA uliofanyika uwanja wa Igoma Stendi ukiongozwa na Makamu mwenyekiti John Heche pamoja wanachama wengine wa chama hicho.
Naye Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA John Heche katika hotuba yake kwa wakazi wa Mwanza ameiomba serikali kushughulikia changamoto ya ajira kwa vijana kutokana na ongezeko kubwa la vijana wasio na ajira
Hata hivyo Bw. Heche amewataka wanachama wa chama hicho kutotishwa na walioshindwa mapambano na kuondoka kisa CHADEMA haishiriki uchaguzi bila mabadiliko kufanyika.