Jamii wilayani Ngara mkoani Kagera imetakiwa kuendelea kutunza mazingira kwa kupanda na kulinda misitu ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi yanayoikumba dunia.
Amesema hayo kwa niaba ya mkuu wa wilaya, afisa tarafa Nyamiaga Jawadu Yusuph wakati wa zoezi la upandaji miti lilifanyika shule ya msingi nyamikono kijiji cha Mshikamano kata ya Rusumo na kutaka zoezi hilo la upandaji miti lisiishie shuleni tu bali liendelee hata kwenye eneo la kijiji hicho.
Jawadu amesema utunzaji miti unasaidia kutunza mazingira yetu na kupunguza hewa ukaa.
Wiki ya Misitu duniani huadhimishwa march 23 kila mwaka na kauli mbiu mwaka huu ni Misitu ni uchumi.
