
Na, Zawadi Bashemela
LIBREVILLE
Jenerali Brice Nguema ameibuka mshindi wa kiti cha Urais nchini Gabon, kufuatia uchaguzi uliofanyika Jumamosi Aprili 12, 2025.
Uchaguzi huo ulikuwa wa kwanza wa Rais tangu Jeshi la Gabon lilipomwondoa madarakani Rais Ali Bongo Ondimba mwaka 2023.
Kwa mujibu wa matokeo ambayo yamekwishatangazwa mpaka sasa, Jenerali Nguema amepata asilimia 90.35 ya kura zote zilizopigwa.
Mpinzani wake mkuu Alain-Claude Bilie By Nze amepata asilimia tatu ya kura, huku wagombea wengine sita hawakuvuka asilimia moja ya kura.
Jenerali Oligui ndiye aliyemaliza utawala wa familia ya Bongo uliodumu kwa muda wa zaidi ya miaka 50 mwezi Agosti mwaka 2023, na kuwa Rais wa mpito wa Taifa hilo.