
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limekamata shehena ya Mirungi ambayo ilikuwa ikisafirishwa kutoka nchi jirani kwa njia ya bahari, katika eneo la Mawe Mawili lililoko Kijiji cha Kwale wilayani Mkinga mkoani humo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi ameeleza kuwa dawa hizo zilikuwa zikisafirishwa kwa boti ambayo imekamatwa usiku wa kuamkia leo Julai 22, 2025, na watuhumiwa wametoroka.
Kamanda Mchunguzi ameongeza kuwa Jeshi la Polisi mkoani Tanga linaendelea kuwasaka watuhumiwa hao ili waweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.