
Jeshi la Polisi mkoani Mara linamshikilia Jumanne Kibagi mkazi wa kijiji cha Nyarufu wilayani Bunda kwa tuhuma za kumuua mama mkwe wake sambamba na kumjeruhi mke wake kwa kuwakata na panga.
Kibagi anatuhumiwa kumuua mama mkwe wake Kabula Masanja (50) mkazi wa Kijiji cha Chumwi wilayani Musoma na kumjeruhi mke wake Nyageta Alex (21).
Akizungumza leo Julai 22,2025 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere alikolazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu, Nyangeta amesema tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Chumwi wilayani Musoma usiku wa Julai 19,2025.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Pius Lutumo amekiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba tayari jeshi hilo linamshikilia mtuhumiwa huyo kwa uchunguzi zaidi.