Msanii wa Bongo Fleva Juma Jux ameandika historia nyingine nchini Nigeria baada ya kupanda jukwaani kwa style ya kipekee, akiwa amefungwa kamba (rope entrance) wakati wa shoo yake kubwa jijini Lagos.
Entrance hiyo imekuwa gumzo kubwa mitandaoni, kiasi kwamba blog moja kubwa ya Nigeria imeandika kuhusu tukio hilo na kuchochea maelfu ya maoni kutoka kwa wasomaji wake.
Kwenye video iliyotembea sana, mashabiki wa Nigeria wameonyesha kuvutiwa na ubunifu, ujasiri na maandalizi ya Jux, wakisema ameleta kiwango kipya cha performance nchini humo. Maoni mengi yamejaa sifa, huku baadhi wakisema “Juma Jux ni wa kwanza kuleta style hii Nigeria” na wengine wakimpa heshima ya “Mkwe Wa Mwaka” wakimaanisha namna alivyoheshimu jukwaa la Nigeria.
Wengi pia wamesisitiza kuwa Jux hutoa kila kitu jukwaani, na bidii yake inaonyesha anavyoichukulia kazi yake kwa uzito mkubwa. Mapokezi haya yanaonyesha wazi kuwa Lagos haikumkaribisha tu Jux, bali imemkubali rasmi.