
Wakazi wa mtaa wa Mwatulole manispaa ya Geita mkoani Geita wamelaani kitendo cha kutupwa kwa kichanga ambacho kimekutwa kimeungua na moto ambao umeunguza eneo hilo
Wakazi hao wamesema aliyetenda tukio la kutupa kichanga hicho bado hajafahamika wala aliyechoma moto eneo hilo
Wameomba uongozi wa mtaa wa kufanya uchunguzi na kubaini mhusika ili hatua ziweze kuchukuliwa
Redio kwizera inaendelea na juhudi za kulipata jeshi la polisi kwaajili ya ufafanuzi wa tukio hilo