
Na, Zawadi Bashemela
MVOMERO
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ismail Ali Ussi amewataka wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kuachana na matumizi ya kuni na mkaa bali wajikite kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kutimiza azma ya serikali ya kutunza na kulinda mazingira.
Ametoa kauli hiyo wakati akizindua mradi wa nishati safi ya kupikia Shule ya Sekondari Mzumbe ambapo amewataka wananchi kuona umuhimu wa kuunga mkono jitihada za serikali ili kuwa na mazingira salama.
Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Kilimo Misitu, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali linalotekeleza mradi wa kilimo misitu, Deogracius Ignas amesema tangu mradi huo ulivyoanza kutekelezwa, zaidi ya miti laki sita imepandwa katika maeneo mbalimbali, mradi ukigharimu zaidi Shilingi Milioni 100.