Staa wa muziki kutoka Nigeria, Kizz Daniel, amejizawadia zawadi ya Krismasi mapema kwa kununua jumba la kifahari pembezoni mwa bahari huko visiwani Zanzibar.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kizz Daniel ameshare picha za nyumba hiyo ya kifahari, akieleza kuwa ni zawadi maalum aliyojipa yeye pamoja na familia yake, huku akibainisha kuwa jumba hilo litakuwa nyumba ya mapumziko (vacation home).
“Xmas came early my gift to myself and my family this Xmas VACATION HOME IN ZANZIBAR, TANZANIA 🇹🇿,” ameandika Kizz Daniel.
Hitmaker huyo wa Buga ameongeza shukrani kwa mashabiki wake kwa mwaka mzuri uliojaa mafanikio, akisema: “Thank you guys for a GOOD YEAR.”
Hatua hiyo inaonesha sio tu mafanikio yake makubwa katika muziki, bali pia mapenzi yake kwa Tanzania, hususan Zanzibar, ambayo imeendelea kuvutia mastaa wa kimataifa kama kituo cha mapumziko na uwekezaji.