
Kadinali Giovanni Battista Re, mwenye umri wa miaka 91, ndiye Kiongozi Mkuu wa Makadinali kwa sasa, na mshiriki mkuu zaidi kwenye jopo la Makadinali ambao hushiriki mchakato wa kumchagua Papa mpya.
Kwa hali ya kawaida, Giovanni angehakikisha mchakato wa kongamano la kumchagua Papa mpya unaenda vyema mara tu utakapoanza Mei 7, 2025.
Hata hivyo, kwa sababu ya umri Kadinali Giovanni hatoshiriki Kongamano hilo pamoja na Makamu wake Mkuu, Kadinali Leonardo Sandri.
Hivyo mkutano ujao utaongozwa na Kardinali Askofu Pietro Parolin, ambaye kwa sasa ni katibu wa serikali ya Vatican.
Kwa karne nyingi sasa, mwongozo na mchakato wa kumchagua Papa mpya hufanywa na Makadinali wenye umri wa chini ya miaka 80 wanaokadiriwa kuwa 135.
Hii ni idadi kubwa ya Makadinali wenye umri wa chini ya miaka 80 watakao pia kura ya kumchagua Papa katika historia ya Kanisa Katoliki.
Na hii inatokana na uteuzi mkubwa wa makadinali wapatao 108 wenye umri stahiki wa kupiga kura uliofanywa na Papa Fransisco wakati wa uhai wake.
Ikumbukwe Papa Fransisco alifariki mnamo tarehe ya 21 Aprili 2025 akiwa na umri wa miaka 88 na kuzikwa katika Basilika ya Maria Mkuu mnamo tarehe 26 Aprili 2025.