
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa wito kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kujitokeza hadharani na kutoa kauli zake binafsi kuhusu maandalizi ya uchaguzi na dhamira ya kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki, badala ya kauli hizo kutolewa kwa niaba yake na serikali au chama tawala.
Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Fulgence Massawe, wakati akizungumza na wanahabari
Kwa mujibu wa LHRC, kitendo cha serikali kuendelea kuwa msemaji mkuu wa masuala ya uchaguzi ni dalili ya ukosefu wa uhuru wa tume hiyo na kinaibua maswali kuhusu imani ya wananchi katika mchakato wa uchaguzi.
LHRC ni miongoni mwa taasisi zinazofuatilia haki za kiraia na uchaguzi nchini Tanzania, na imekuwa mstari wa mbele katika kushinikiza mageuzi ya kweli ya kikatiba na ya kisheria ili kuwezesha uchaguzi huru, wa haki, na unaokubalika na wadau wote.