Msanii wa Uganda, Mad ice amerejea jijini Dar es Salaam kwa mara nyingine tangu mwaka 2019, ikiwa ni kipindi cha miaka sita tangu ujio wake wa mwisho.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mad Ice amezungumzia safari yake ya muziki, akiweka mkazo kwenye albamu yake maarufu “Baby Gal”, yenye nyimbo zilizotikisa miaka ya 2004 – 2005, ikiwemo wimbo wa “Baby Gal” uliompa umaarufu mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Aidha, msanii huyo amethibitisha kuwa ataanza ziara ya vyombo vya habari hivi karibuni, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uhusiano wake na mashabiki wa Tanzania.
Pia ameeleza kufurahishwa na jinsi muziki wa Afrika Mashariki umeendelea kukua, huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wasanii wa kanda hii ili kupeleka muziki wa ukanda huo kimataifa zaidi