Samwel Masunzu- Kibondo, KIGOMA
Makamu Askofu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God T.A.G jimbo la Kigoma Kaskazini mchungaji Robert Luhumbi amewataka waumini wa Kanisa hilo kuweka malengo na kutenga muda katika utumishi ndani na nje ya Kanisa.
Mchungaji Luhumbi ambaye anatumikiwa kanisa la T.A.G AGAPE Kibondo mjini amesema hayo wakati wa kuhitimisha somo ambalo amelifundisha kwa kipindi cha wiki tatu linalohusu βUmuhimu wa Mungu kutembea na Mwanadamu”
Amesema ili kufikia malengo ndani ya kanisa na mafanikio ya kiuchumi, kila mmoja anapaswa kutenga mahali pa kutumika ndani ya nje ya kanisa badala ya kuwa waumini wasio na sehemu ya utume.
Aidha amesema kuwa, kiu yake ni kuona waumini wote wakifanikiwa katika mipango yao ya mwaka 2026

Hata hivyo mchungaji Luhumbi amewakata waumini wa kanisa hilo kuendelea kuwa na utii, uadilifu na kumtegemea Mungu katika kila jambo wanalolifanya na kwamba ili kufikia malengo lazima kuwe na utii, uadilifu na kumheshimu Mungu pamoja na viongozi.
Moja ya malengo ya kanisa hilo ni kuhamasisha kila muumini kuwa na shuguli ya kufanya katika kuongeza kipato na kusimulia matendo makuu ya Mungu mwishoni mwa mwaka ikiwa ni mafanikio ya malengo ya mwaka mzima.

