Mbunge wa Arusha Mjini na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda amesema kuna mpango wa kuiboresha barabara inayounganisha Moshi na Arusha hadi kuwa ya njia nane, mradi unaotarajiwa kutekelezwa kwa ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi (PPP).
Ametoa kauli hiyo wakati Akizungumza katika kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Arusha kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Gabriel Makalla.
Makonda ameeleza kuwa barabara hiyo itatoa fursa kwa magari ya kawaida kutumia njia za kawaida huku magari ya mwendokasi yakipata njia maalum za kupunguza msongamano.
Hata hivyo Amesema uboreshaji huo utasaidia kufungua uchumi wa Kanda ya Kaskazini kwa kurahisisha usafiri wa watu, mizigo na watalii.
