Enock Yoronimo- Bukoba, KAGERA
Makundi maalumu ya wazee, wenye ulemavu pamoja na wanufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika Kata ya Kibeta Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera yamepatiwa msaada wa vyakula ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kipindi cha mfungo wa Ramadhanin na Kwaresima
Msaada huo wa chakula umetolewa na Katibu wa Mbunge Ahamada Simba kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini Mhandisi Johnstone Mutasingwa ambapo amesema lengo ni kuwafikia wananchi walioko kwenye mazingira

Wananchi waliopokea msaada huo wamesema chakula hicho kitawasaidia katika kusherekea huku wakieleza kuwa msaada huo umekuja kwa wakati muafaka na kwamba wamepata faraja katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa mfungo wa Ramadhani na Kwaresma.
Kitendo hicho kimeyafanya makundi hayo kupata faraja pamoja na kuimarisha uhusiano kati ya viongozi na wananchi kwaajili ya Maendeleo endelevu.

