Watu watatu, wamekamatwa na askari wa maliasili wilayani Tanganyika Mkoani kwa tuhuma za kujihusisha na kilimo cha bangi ndani ya hifadhi ya misitu ya kijiji cha Kapanga.
Watuhumiwa hao wanadaiwa kulima zao hilo katika eneo la takribani hekta tisa akiwemo mwanamke mwenye umri wa miaka 65.
Askari wa maliasili walifanya operesheni maalumu na kuyateketeza mashamba hayo ili kulinda misitu ya hifadhi na uwekezaji wa biashara ya hewa ya ukaa (Carbon) unaotekelezwa katika eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu, amewataka wananchi kuthamini na kulinda biashara ya hewa ya ukaa, kwasababu ina manufaa ya kijamii ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule na hospitali.
Baadhi ya wananchi wamesema wanachukizwa na vitendo vya kilimo cha bangi, kinahatarisha maendeleo ya jamii na kunufaisha watu wachache na kurudisha nyuma maendeleo.