
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, amezitaka mamlaka za maji nchini kuvitunza vyanzo vidogo vya maji kama suluhisho mbadala pale miradi mikubwa inapokumbwa na changamoto.
Akizungumza Septemba 16, 2025, wakati akikagua ujenzi wa chujio la maji lenye uwezo wa kuchuja lita milioni 10 kwa siku katika eneo la Mwendakulima, Kahama, Mhandisi Mwajuma alisema hatua hiyo ni muhimu kwa usalama wa huduma kwa wananchi.
Aidha, amesifu kazi ya usanifu wa mradi huo iliyofanywa na wataalamu wa ndani, akihimiza wahandisi wazawa kutumia miradi kama hii kujijengea uwezo na uzoefu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazinfgira Kahama, (KUWASA) Allen Marwa, alisema mradi unalenga kuhakikisha huduma ya maji inapatikana hata wakati wa dharura, na unatarajiwa kukamilika Februari 2026