Msanii wa Bongo Fleva Marioo ameendelea kuonyesha ukubwa wa kisanii kupitia The Godson – Deluxe Edition, hii ikiwa ni toleo linalounganisha mafanikio na tafakari. Ndani ya albamu hii, mashabiki tayari wamesikia nyimbo kama Tete, Mvua, Ha Ha Ha na Dunia, ambazo zimekuwa hits kubwa za mwaka huu, zikimtambulisha Marioo kama mmoja wa wasanii waliotawala masikio ya wengi 2025.
Lakini umakini wote sasa unahamia kwenye “#Oluwa”, wimbo pekee mpya ndani ya toleo hili la Deluxe. Tofauti na nyimbo nyingine zilizosikika, Oluwa inakuja kama sauti mpya masikioni mwa mashabiki, ikifunga hesabu za The Godson, albamu ya pili ya @marioo_tz ambayo wachambuzi waliita maana halisi ya muziki wa Afrika Mashabiki.
Kwa mpangilio huu, Marioo hajaongeza tu wimbo, amekamilisha simulizi. #TheGodsonDeluxe inakuwa daraja kati ya mafanikio yaliyopita na ujumbe mpya unaomuacha msikilizaji aamue.
“Oluwa” ni wimbo uliobeba hatma ya Albamu hii ikithibitisha kuwa wakati mwingine, sauti moja mpya inatosha kufunga safari nzima.