
Jumla ya Miradi ya Maendeleo 58 yenye thamani ya shilingi bilioni 23.8 itazinduliwa , Kukaguliwa , kutembelewa na kuwekewa mawe ya msingi na Mwenge wa Uhuru katika mkoa wa Kagera ambao umeanza kukimbizwa leo Septemba 7.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa amesema hayo baada ya kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela ambapo mapokezi ya Mwenge huo yamefanyika katika kata ya Nyakabango Wilaya ya Muleba ukitokea mkoani Geita.
Hajjat Mwassa amesema kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa mkoani Kagera utakimbizwa katika halmashauri zote 8 za mkoa huo kwa umbali wa kilometa elfu 1 na 40 na kwa mwaka 2024 Mwenge wa Uhuru ulitembelea, kukagua,Kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye Jumla ya miradi 55 yenye thamani ya shilingi bilioni 53.9.
Naye kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025 Ismail Ali Ussi wakati akizindua mradi wa Barabara ya Katembe Mwaloni yenye urefu wa Kilometa 0.56 kwa kiwango cha Lami amesema kuwa utekelezaji wa miradi hiyo ni kutokana na dhamila na maono ya Serikali ya kuhakikisha maendeleo hayo yanafanyika kila eneo.