
Leo Jumatatu Aprili 28, 2025 Makardinali waliopo mjini Roma wamefanya uamuzi kuwa mkutano wa kumchangua Papa mpya utaanza Mei 7, 2025.
Kulingana na Ofisi ya Habari ya Vatican, Wamesema Mkutano wa kumchagua utafanyika katika Kanisa la Sistine la Vatican, ambalo limefungwa kwa ajili ya wageni husika kwa siku hizo zilizopangwa.
Mkutano wa kuamua tukio hilo umekuwa ni Mkutano wao Mkuu wa tano tangu Baba Mtakatifu Francisko alipofariki dunia Aprili 21, 2025.