
Wananchi wilayani Ngara mkoani Kagera wametakiwa kuzingatia taratibu za utatuzi wa migogoro ya ardhi ili kuzifikia haki zao.
Hayo yamesemwa na Mwanasheria kutoka timu ya Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Bw. Shafii Abdul ambaye pia ni mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara.
Bw. Shafii amesema mabaraza ya Ardhi ya Kijiji na Kata yapo kwa lengo la kutoa Suluhu huku Baraza la Ardhi la wilaya ni kwa ajili kutoa hukumu.
Aidha Bw Shafii wakati akitoa elimu hiyo katika Kata ya Mulukurazo wilayani humo amesema iwapo mtu hajaridhika na huku anaweza kukata rufaa kwenda Mahakama Kuu na mwisho ni Mahakama ya rufaa ya Tanzania.
Timu ya Msaada wa Kisheria ya ‘Mama Samia Legal Aid’ inaendelea na Kampeni ya kutoa elimu na msaada wa kisheria kwenye vijiji 30 ndani ya kata 10 za wilaya ya Ngara.