Mwendesha pikipiki Stefano Maziku (25), mkazi wa Igwesa, Kijiji cha Iboja, wilaya ya kipolisi Ushetu mkoani Shinyanga, amekutwa ameuawa kisha mwili wake kutelekezwa na watu wasiojulikana
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo Novemba 16, 2025 na kwamba Jeshi la Polisi linawasaka wahusika wa tukio hilo.
Aidha Magomi amesema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni kuwania mali kwani baada ya wahalifu kutekeleza tukio hilo walitoweka na pikipiki ya marehemu.
Mauaji ya waendesha Pikipiki maeno mablimbali yamekuwa yakiripotiwa na kusisitizwa kuzingatia usalama wao wakati wa shughuli zao kwa kuepuka kusafirisha abiri wasio wajua usiku na maeno yasiyo salama kwao.