
Mbio za mwenge wa uhuru 2025 zinatarajia kupitia na kukagua miradi 61 yenye tahamani ya shilingi bilioni 164.4 mkoani Geita ikiwa ni ongezeko la zaidi ya asilimia 500 ya thamani ya miradi iliyopitiwa na mwenge wa uhuru kwa mwaka jana 2024 mkoani humo
Mwenge wa uhuru kwa mara ya kwanza kabisa uliwashwa mwaka 1961 katika kilele cha mlima Kilimanjaro dhumuni ni kumulika ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, kuleta matumaini pale ambapo kuna kukata tamaa, upendo mahali penye chuki na heshima mahali penye dharau
Kwa mkoa wa Geita mbio za mwenge wa uhuru zinaanza Septemba 1 ambapo zitapokelewa katika kijiji cha Lwezera wilaya ya Geita baada ya kutoka mkoa wa Mwanza
Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela amesema miradi itakayopitiwa na mwenge ni 61 yenye thamani ya Zaidi ya sh. bilioni 164.4
Shigela amesema ongezeko la miradi na thamani ni kutokana na kazi ambayo inafanywa na serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
Kaulimbiu ya mbiu ya mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu ni “Jitokeze kushirki uchaguzi mkuu 2025 kwa amani na utulivu” na hii ni kutokana na zoezi la uchaguzi wa Rais , wabunge na madiwani oktoba 29