Msanii mkongwe kutoka Kenya, Nameless, ameonesha heshima na upendo mkubwa kwa msanii wa Tanzania, Marioo, kufuatia kushirikiana kwao kwenye wimbo wa “Nasinzia II.”
Kupitia ujumbe wake, Nameless amesema amefurahia sana kufanya remix hiyo na kumtaja Marioo kama “brother ake wa Tanzania,” akisisitiza kuwa ameleta vibe mpya inayopendwa zaidi na kizazi cha sasa.
Mbali na kumpongeza Marioo, Nameless pia ameishukuru Afrika Mashariki kwa sapoti waliompa kwa miaka mingi, akisema: “East Africa, thank you for the many years of love you have shown me and my songs! Keep watching, keep sharing and keep making sweet memories! THIS IS FOR THE LOVERS IN THE HOUSE!!!”
Ujumbe huo umepokelewea vizuri na mashabiki, kauli ya “Hapo sawa King!!!” ni ishara ya heshima na kuthamini mchango wa Marioo kwenye remix hiyo.
