Binti wa Kim Kardashian na Kanye West, North West, mwenye umri wa miaka 12, ameteka vichwa vya habari mitandaoni kutokana na mtindo wake wa kuishi.
Watu wanamtuhumu kwa kufuata mfano wa mama yake na The Kardashian, North alionekana na tatoo za bandia usoni, nywele zenye rangi ya buluu, lensi za macho ya buluu, na mapambo ya mikono ya henna.
Hata hivyo, baba yake, Kanye West (Ye), hakuwa na furaha na mabadiliko haya na Kanye alionyesha wasiwasi wake kwa Kim Kardashian, akihisi kuwa binti yao anahimizwa kukua kwa haraka sana, na akilaumu mtindo huo kama.
Hii ni sehemu ya tofauti zinazoendelea kati ya Kanye na Kim kuhusu jinsi ambavyo picha ya mtoto wao inavyowasilishwa.