Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania, CPA (T) Nyakaho Mahemba, ametoa wito kwa wanufaika na watakaonufaika na mikopo ya Serikali kupitia Mfuko huo kuhakikisha wanarejesha kwa wakati.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam, wakati wa Mafunzo kwa Watengenezaji wa Maudhui Mtandaoni yaliyoandaliwa na Wizara kupitia Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, likilenga kuongeza uelewa kuhusu mikopo, uwajibikaji na namna ya kutumia fursa hizo kwa ufanisi.
Mahemba alisema kuwa urejeshaji wa mikopo hiyo ni muhimu ili Mfuko uweze kuendeleza miradi ya utamaduni na sanaa, pamoja na kutoa msaada kwa wasanii na watengenezaji wa maudhui wa mtandaoni.
Pia amesema wito huo ni sehemu ya kuhakikisha uwajibikaji na matumizi sahihi ya rasilimali za umma.
