Msanii na mdau mkubwa wa burudani nchini Marekani Sean John Combs aka P. Diddy, amepewa tarehe mpya ya kutoka jela ambayo ni April, 25, 2028.
Amepunguziwa siku baada ya kukubali kushiriki programu tofauti ya kurekebisha tabia ikiwepo matumizi ya dawa za kulevya.
Diddy anatumikia kifungo cha miaka minne baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha watu kwa ajili ya shughuli za ngono.
