
Serikali kupitia Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), imesema kuwa imeendelea kuimarisha mifumo ya usimamizi na uagizaji mafuta nchini.
Akizungumza katika mkutano na Wahariri pamoja na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa PBPA, Erasto Simon, amesema Serikali imeweka kipaumbele katika utekelezaji wa sera ya nishati inayolenga upatikanaji wa nishati safi, salama na ya uhakika kwa wananchi wakati wote.
Aidha Bw. Simon ameeleza kuwa kwa kushirikiana na wizara na taasisi mbalimbali, Serikali imeboresha mifumo ya kifedha ili kuwawezesha wafanyabiashara wa mafuta kulipia kwa wakati kupitia mfumo maalum wa uagizaji wa mafuta.
Aidha amesema, Serikali imefanya maboresho katika mikataba ya uletaji wa mafuta ili kuwapa fursa wafanyabiashara kutumia njia mbadala za malipo badala ya kutegemea Dola pekee, hatua inayolenga kuongeza unafuu na ufanisi katika upatikanaji wa mafuta nchini.