
Dodoma
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Palamagamba Kabudi amesema Serikali imefanikiwa kutambua na kuenzi lugha adhimu ya Kiswahili kama lugha muhimu kimataifa………
Profesa Kabudi ameyasema hayo wakati akieleza mafanikio ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika kipindi cha miaka minne katika mkutano wake na waandishi wa habari leo Jijini Dodoma…..
Amesema hatua hiyo ilifuata baada ya mkutano mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) katika kikao chake kilichofanyika mwezi Novemba mwaka 2021 nchini Ufaransa na kupendekeza Julai 7 kuenzi lugha hii adhimu…..