
Rais wa Urusi Vladimir Putin yuko tayari kushiriki katika juhudi za kuleta amani nchini Ukraine, lakini siyo haraka kama Washington inavyotarajia.
Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov, amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa malengo ya kimkakati ya Urusi lazima yatimizwe, na Moscow inapendelea kuyafikia kwa njia ya amani.
Aliongeza kuwa Rais Putin ameonesha utayari wa kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na uongozi wa Ukraine, lakini hadi sasa hakuna jibu lolote kutoka Kyiv.
Rais wa Marekani, Donald Trump, ambaye amekuwa akijitambulisha kama mpatanishi wa amani, mara kwa mara ametamka nia yake ya kukomesha “umwagaji damu” unaoendelea katika vita hivyo vya zaidi ya miaka mitatu.
Hata hivyo, shirika la habari la TASS lilimnukuu Peskov akisema kwamba mizizi ya mzozo wa Ukraine ni tata mno kiasi kwamba haiwezi kutatuliwa kwa siku moja tu.