
Serikali wilayani Bukoba mkoani Kagera imesema kuwa itawachukulia hatua za kisheria, wananchi wote watakaobainika kuwapokea na kuwatumia katika shughuli mbalimbali raia wa kigeni, wanaoingia nchini kinyume na sheria.
Mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Sima ameeleza hayo baada ya kubainika raia 13 wa kigeni walioingia wilayani humo kinyume na utaratibu, na kuajiriwa kwenye mashamba na kazi za ndani kwa watu.
Amesema kuwa vitendo vya kuwapokea raia wa kigeni wanaoingia nchini kwa ajili ya shughuli hizo ni kinyume na sheria na kwamba jeshi la polisi, maafisa uhamiaji na viongozi wa serikali wanaendelea kuwafuatilia raia wa kigeni 7 waliotoroka ili waweze chukuliwa hatua
Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Bukoba Beatrice Shangwe na Najim Ashim wamesema kuwa raia hao wa kigeni hutumiwa katika shughuli mbalimbali kutokana na unafuu wa malipo baada ya kufanya kazi.
Hata hivyo wameahaidi ushirikiano kwa serikali kuwafichua watu wanaowapokea raia hao wa kigeni wasiofuata taratibu za kuingia nchini