
Rais Samia Suluhu Hassan, kesho Agosti 9, 2025, anatarajiwa kuchukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Jijini Dodoma.
Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla, ameeleza hayo jijini Dodoma na kuongeza kuwa Rais Samia atafuatana na mgombea mwenza wake, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa CCM.
Baada ya kuchukua fomu, Rais Samia ataelekea katika ofisi za CCM Dodoma kuhutubia wanachama wa chama hicho.
Ikumbukwe Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza ratiba ya uchaguzi mkuu mwaka huu, ambapo uchaguzi huo umepangwa kufanyika Oktoba 29, 2025.