
Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, ametoa ameshauri kufanyika mazungumzo ya kitaifa kati ya Serikali na vyama vya siasa ili kutatua mzozo kuhusu mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa uchaguzi nchini Tanzania.
Akizungumza kuhusu mvutano unaoendelea kati ya Serikali na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) juu ya madai ya katiba mpya na kauli ya “No Reform, No Election”, Wakili Mwabukusi amesema muda wa kufanya mabadiliko bado upo na hakuna linaloshindikana katika meza ya mazungumzo.
Ameonya kuwa ni hatari kwa Taifa iwapo mivutano ya kisiasa itaendelea kuchochewa na matamko ya kichochezi yanayoweza kusababisha vurugu na madhara kwa raia.