
Rais wa Kenya, William Ruto amewaomba msamaha Watanzania na Waganda kama kuna jambo lolote ambalo nchi hiyo imekosea.
Rais Ruto ameyaomba radhi mataifa hayo leo Jumatano, wakati wa Ibada Maalumu ya kuliombea taifa hilo iliyofanyika eneo la Safari Park nchini humo.
Akinukuu Biblia Akinukuu Maandiko Matakatifu ya Biblia kutoka kwenye Zaburi 133 inayosisitiza kuhusu ndugu kuishi pamoja kwa umoja, Ruto amesema nchi yoyote isiyo na shukurani kwa kidogo inachopata basi haitoshukuru hata ikipata mafanikio makubwa, huku akiwataka raia wa nchi hiyo kuungana na kuwa kitu kimoja.
Aidha Rais Ruto, ameihakikishia Tanzania kuwa Kenya imejikita katika kudumisha uhusiano mzuri wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, kufuatia tukio la hivi karibuni ambapo wanaharakati kadhaa wa Kenya waliripotiwa kukamatwa na kurejeshwa Kenya.